Chemka Luxury Villas Logo CHEMKA LUXURY Villas
  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Kuhusu Sisi
    • Picha
    • Maswali Yanayoulizwa
    • Vigezo na Masharti
    • Sera ya Faragha
  • Malazi
  • Uzoefu
  • Makala
  • Weka Booking
Weka Booking
Faragha & Data

Sera ya Faragha

Yaliyomo

  • 1. Utangulizi
  • 2. Data Tunazokusanya
  • 3. Matumizi ya Data
  • 4. Cookies & Kufuatilia
  • 5. Ulinzi wa Data
  • 6. Haki Zako
  • 7. Wasiliana Nasi

01 Utangulizi

Chemka Luxury Villas imejitolea kulinda faragha ya wageni wake na watumiaji wa tovuti hii. Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kufichua, na kulinda taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu au kuweka nafasi ya kukaa kwetu.

02 Data Tunazokusanya

Tunakusanya aina zifuatazo za taarifa binafsi ili kuwezesha huduma bora:

  • Taarifa za Mawasiliano: Jina kamili, barua pepe, namba ya simu, na nchi unayotoka.
  • Taarifa za Uhifadhi: Tarehe za kuwasili na kuondoka, aina ya villa iliyochaguliwa, na mahitaji maalum.
  • Data ya Kifaa na Matumizi: Anwani ya IP, aina ya kifaa (Simu au Kompyuta), na kurasa unazotembelea kwenye tovuti yetu kupitia mfumo wetu wa usalama na ufuatiliaji wa takwimu.

03 Jinsi Tunavyotumia Data Zako

Tunatumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kusindika na kudhibitisha maombi yako ya booking na reservation.
  • Kutuma barua pepe za uthibitisho au mawasiliano kuhusu kukaa kwako.
  • Kuboresha huduma za tovuti yetu na kuboresha uzoefu wa mtumiaji.
  • Kufuata matakwa ya sheria za nchi ya Tanzania.

04 Cookies & Teknolojia za Kufuatilia

Tovuti yetu inatumia cookies kuhifadhi lugha uliyochagua (Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza au Kiebrania) na kufuatilia takwimu za jumla za utembeleaji wa tovuti yetu. Unaweza kuzuia cookies kupitia mipangilio ya kivinjari (browser) chako, lakini hii inaweza kuathiri utendaji wa baadhi ya kurasa.

05 Ulinzi na Usalama wa Data

Tunachukua hatua madhubuti za kiufundi kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya upotevu, wizi, au ufikiaji usioruhusiwa. Mawasiliano yote ya tovuti yetu yanalindwa kwa teknolojia ya encryption ya SSL.

Hatuuzi au kukodisha taarifa zako binafsi kwa watu wengine kwa madhumuni ya masoko (marketing).

06 Haki Zako za Faragha

Una haki zifuatazo kuhusu data zako tunazozihifadhi:

  • Haki ya kuomba kuona taarifa binafsi tulizonazo kukuhusu.
  • Haki ya kurekebisha taarifa ambazo sio sahihi.
  • Haki ya kuomba kufutwa kabisa kwa taarifa zako kutoka kwenye mifumo yetu (isipokuwa zile zinazohitajika kisheria).

07 Wasiliana Nasi

Kama una maswali au unataka kutumia haki zako za faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa:

Barua Pepe: info@chemkaluxuryvillas.com

READY TO ESCAPE?

Experience the Magic of Chemka Springs

Book Your Stay
Chemka Luxury Villas
CHEMKA LUXURY VILLAS

Where Kilimanjaro meets the springs

A sanctuary of refined luxury nestled among the natural thermal springs at the foot of Mount Kilimanjaro, Tanzania.

Chunguza

  • Mwanzo
  • Malazi
  • Uzoefu
  • Picha
  • Makala za Kusafiri

Taarifa

  • Kuhusu Sisi
  • Wasiliana Nasi
  • Maswali Yanayoulizwa
  • Vigezo na Masharti
  • Sera ya Faragha

Mawasiliano

  • Boma Ng'ombe, Kilimanjaro , Tanzania
  • info@chemkaluxuryvillas.com
  • +255 754 395 141
  • WhatsApp Us

© 2026 Chemka Luxury Villas. Haki zote zimehifadhiwa.

Terms · Privacy · Contact

Designed & Developed by MultiTech